Publications

Simulizi ya kweli ya Ghati na Rhobi

Simulizi ya kweli ya Ghati na Rhobi

Simulizi ya Kweli ya Ghati na Rhobi ni filamu ya uhuishaji ya dakika tano inayolenga kuongeza uelewa juu ya ukeketaji. Inaeleza simulizi ya kuvutia ya wasichana wawili (Ghati na Rhobi) ambao walikaataa ukeketaji kwenye jamii yao. Wasichana hawa walionyesha ujasiri kwa kusema hapana kwa ukeketaji, kitendo ambacho walisikia kina maumivu makali ambapo wasichana kadhaa hufariki kutokana nacho. Kwa msaada wa wazee katika jamii yao, walibadilisha mitazamo juu ya kipindi cha mpito cha msichana kutoka usichana kwenda utu uzima yaani kuwa mwanamke kwa kutokomeza ukeketaji.